Waziri  
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akihutubia katika
 Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni 
Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya 
Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, 
Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi 
Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
Ofisa wa Polisi Hamad akikabidhiwa zawadi na Waziri Nchemba.
Askari wa
 Kikosi cha Usalama Barabarani Sajeni, Moses Alphance Sinyagwa 
akipongezwa baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki kutokana na 
ufanyakazi bora.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa neno la shukurani katika maadhimisho hayo.
Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakiwa katika shindano ya kumkamata kuku kwenye maadhimisho hayo.
Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa polisi waliotunukiwa vyeti.
Hapa Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na wadau 
kutoka akampuni yaliyodhamini maadhimisho hayo.
Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
Askari polisi, jamaa zao na waandishi wa habari  wakiwa kwenye hafla hiyo.
-------------------
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa
 Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea 
kupambana wa waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.
Mwigulu 
alitoa kauli hiyo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya 
Familia ya Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo ambapo 
alikuwa mgeni rasmi.
"Serikali
 imejipanga  kupambana na dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la 
kitaifa ambapo vijana wengi wanakuwa waanga wakubwa'' alisema Mwigulu.
Mwigulu 
alisema serikali ya awamu ya tano haitamfumbia macho mtu yeyote atakaye 
kwamisha jitihada za kupambana na uhalifu nchini ambao wamepanga 
kuupunguza kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2019.
Aliongeza
 kuwa kanuni na sheria zilizowekwa na mkoloni ambazo zinazotumika ndani 
ya jeshi la polisi zimekuwa na changamoto kubwa kwa askari polisi. 
Akitolea 
mifano kadhaa alisema askari polisi aliyekosa nyumba ya kuishi ya jeshi 
hilo anapaswa kupewa fedha za kulipia pango nje ya kambi ya polisi na 
suala hilo si la kumuonea huruma askari husika bali ni haki yake.
Alisema 
kwa upande wa askari polisi aliyeumia au kupoteza kiungo wakati wa 
mapambano dhidi yake na wahalifu askari huyo anapaswa kulipa fidia yake 
kwa wakati badala ya kuunda tume ya kuchunguza jinsi alivyoumia akiwa 
katika mapambvano hayo.
"Mambo 
mengine hayahitaji mpaka uwe na elimu kubwa askari amepambana na 
majambazi mbele ya watu lakini majambazi hayo yamemjeruhi fidia yake 
anashindwa kulipwa eti mpaka iundwe tume haya si mambo ya ajabu" alihoji
 Mwigulu.
Alisema 
kwa muda mrefu askari anapopangiwa kituo cha kazi amekuwa akijigharamia 
kwa nauli na fedha za kujikimu kwa zaidi ya miezi mitatu na zaidi bila 
ya sababu za msingi.
Alisema 
hali hiyo kama askari husika anakuwa si mzalendo anaweza kujiingiza 
katika tamaa na kutumia silaha aliyonayokufanya uhalifu hivyo akaomba 
wahusika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwani mshahara na posho kwa 
askari hao ni haki yao.
Mwigulu 
alisema serikali kupitia Rais Dk. John Magufuli imejipanga kuweka 
mazingira mazuri kwa askari polisi ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba 
na kuona namna ya kubadilisha sheria ambazo zinaonekana hazina tija kwa 
wakati huu katika kuliongoza jeshi hilo.
0 comments:
Post a Comment