Rais wa
Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka wafuasi wake rasmi na kuvunja
katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki
shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua
kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza jijini
Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika
Ukumbi wa Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
Bwana
Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki
kwa niaba ya ITV.
Maharusi,
wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya
keki.
Hapa
ilikuwa ni muda wa Kwaito..........
Sehemu
ya wageni waalikwa.....
Wadau
kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha mbele ya
kamera ya Sufiaimafoto.

Baadhi
ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi, wakipozi kwa picha, baada
ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya
Keki.
Sehemu
ya wageni waalikwa,..
Salum
Mkambala, akisebeneka kwa staili yake wakati akielekea kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya
wafanyakazi wenzake wa Chanel Ten.
0 comments:
Post a Comment