KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA GNSM CONTRACORS CO. LTD INAYOENDESHA NA GEOFREY MUNGAI YATOA MSAADA WA CHAKULA CHA MWAKA MPYA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

HAPPY BIRTHDAY YA MAMAA WA MITINDO ASIA KHAMSIN IDAROUS YAFANA KWENYE KIOTA CHA NYUMBANI LOUNGE

DSC_1539 DSC_1543
Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Mamaa wa Mitindo Asia Khamsin Idarous, akizungumza machache kabla ya kukata cake kwenye mnuso wake wa kumbukumbu ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye kiota cha Nyumbani Lounge.
DSC_1541
Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Mamaa wa Mitindo Asia Khamsin Idarous jana alisheherekea siku yake ya kuzaliwa na ndugu, jamaa na marafiki katika mnuso wa nguvu uliofanyika kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam. Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio katika mnuso huo wa nguvu.(Picha zote na MOblog)
DSC_1547
Aunty Asia Idarous akikata ji-cake lake la kutimiza miaka 54 ya kuzaliwa kwake kwenye mnuso wa nguvu uliofanyika Nyumbani Lounge.
DSC_1550
Kata Cake tule......asiyeimba hali...Happy Birthday dear Asia.....Happy Birthday to youuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...!!! We Love Aunty Long Live and Stay Blessed.....Mwaaaaah...!!!
DSC_1553
Mkuu wa kaya ya Nyumbani Lounge Captain Gardner G. Habash alipewa heshima ya kuwa mtu wa kwanza kulishwa cake na Birthday Girl Bi. Asia Khamsin Idarous.
DSC_1575
Mama mwenye nyumba Lady Jay Dee akishow love na Aunty Asia Khamsin Idarous.
DSC_1554
Picha juu na chini ni ndugu, jamaa na marafiki wa Aunty Asia Idarous wakilishwa cake.
DSC_1557
DSC_1559
DSC_1560
DSC_1561
DSC_1562
DSC_1563
DSC_1564
DSC_1565
DSC_1566
Paul Mashauri alikuwa miongoni mwa wadau waliojumuika na Mkongwe wa ubunifu wa mavazi Aunty Asia Khamsin Idarous kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
DSC_1619
Mdau Moddy Bawazir naye aliwakilisha.
DSC_1558
Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda a.k.a Mzee wa Single Button naye alikuwepo.
DSC_1567
DSC_1568
DSC_1620
DSC_1582
Aunty Asia Khamsin Idarous akiserebuka na wadau ndani ya kiota cha Nyumbani Lounge.
DSC_1584
Old is Gold na mimi nimo....Hapana chezea Mamaa wa mitindo.
DSC_1514
Mbunifu wa Mavazi Mustafa Hassanali na wadau wengine wakipata Ukodak na Aunty Asia Khamsin Idarous.
DSC_1532
Aunty Asia Idarous na Ukodak.
DSC_1526
DSC_1538
Aunty Asia Idarous akishow love na binti yake ndani ya nyumbani Lounge.
DSC_1521
DSC_1519
Thank you for coming......love you all....!!

MAMASALMA AMPOKEA MALKIA MAXIMA WA UHOLANZI NA BAADAYE AHUDHURIA DHIFA YA KITAIFA ILIYOANDALIWA NA RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Malkia Maxima wa Uholanzi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 11.12.2013.
 Malkia Maxima wa Uholanzi akipokea ua kutoka kwa kijana mara  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuanza ziara ya siku 3 nchini Tanzania.
 Malkia Maxima akiongozana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiangalia ngoma mbalimbali za utamaduni zilizokuwa zikicheza wakati wa mapokezi ya mgeni huyo Uwanja wa ndege tarehe 11.12.2013.
 Malkia Maxima akiongozana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiangalia ngoma mbalimbali za utamaduni zilizokuwa zikicheza wakati wa mapokezi ya mgeni huyo Uwanja wa ndege tarehe 11.12.2013.
 Malkia Maxima akiongozana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiangalia ngoma mbalimbali za utamaduni zilizokuwa zikicheza wakati wa mapokezi ya mgeni huyo Uwanja wa ndege tarehe 11.12.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha Ikulu, Malkia Maxima wa Uholanzi ili kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 11.12.2013.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu, Malkia Maxima wa Uholanzi kwa ajili ya mazungumzo na dhifa ya kitaifa aliyomwandalia mgeni huyo tarehe 11.12.2013.
Malkia Maxima wa Uholanzi akigonganisha glass/cheers na Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mama Salma wakati wa dhifa ya kitaifa ambayo walimwandalia mgeni huyo huko Ikulu tarehe 11.12.2013. PICHA NA JOHN  LUKUWI

MAELFU WAFURIKA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Picha na 1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Picha na 2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Picha na 3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na 4Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.Picha na 5Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete  akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.Picha na 6 Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.Picha na 7Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu  la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.Picha na 8Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Picha na 9Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.Picha na 10Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”Picha na 11Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya simba kuashiria utalii katika hifadhi  za wanyama za Tanzania.
Picha na 12Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.Picha na 14Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Picha na 15Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini  Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba  aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa  watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.Picha na 16Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na 17Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.Picha na 18Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.Picha na 19Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO