MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 37 YA CCM YAFANA JIJINI MBEYA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Naibu wake (Bara) Mwigulu Nchemba wakati wakimsubiri Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwasili eneola Soweto kuanza matembezi ya mshikamano kuadhimisha miaka 37 ya CCM, leo mjini Mbeya
 Katibu wa NEC, Ogamaizesheni Mohamed Seif Khatib, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakiah Megjj na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Abdallah Bulembo wakibadilishana mawazo wakati wakimsubiri Jk eneo la Soweto kuanza matembezi hayo
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwigulu na Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda wakibadilishana mawazo eneo la Soweto kabla ya matembezi kuanza
 Mkazi wa Mtaa wa Soweto jijini Mbeya akijimwayamwaya wakati akisubiriwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuanza matemebezi hayo
 Wana-CCM wakiselebuka wakati wakimsubiri Mweneyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuwasili eneo la Soweto
 Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili eneo la Soweto kuendesha matembezi hayo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitangaza kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete eneo la Soweto
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Nape namna matembezi yatakavyoanza
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungiamikono wananchi kabla ya matembezi kuanza
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwapungia mkono wananchi matembezi yalipoanza eneo la Soweto. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo huku akiwa na watoto ambao aliwateua kutembea nao baada ya kuwaona eneo la Soweto
 "Haya Simameni Hapa tutembee wote" Rais Jakaya Kikwete akiwaambia watoto hao kabla ya kuanza matembezi
 "Vipi Mmechoka", Rais Kikwete akiwauliza watoto, lakini wakasema hawajachoka ambapo walitembe hadi mwisho umbali wa kilometa tano
 Rais Kikwete akiongoza matembezi hayo
 Wakazi wa Mbeya wakiwa katika shamrashamra za matembezi hayo
 Wafanyabiashara katika soko lililopo karibu na Uwanja wa Sokoine,wakimpungia mkono Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete wakati akipita eneo hilo wakati wa matembezi hayo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasli kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine yalikokomea matembezi hayo
 Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakimlaki Rais Kikwete kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alipowasili kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine mwishoni mwa matembezi hayo
 Mbunge wa Kyela, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimia wananchi mwishoni mwa matembezi hayo
 Mbunge wa Rungwe Mashariki,Profesa Mark Mwandosya akikaribishwa na Nape kusalimia wananchi mwishoni mwa matembezi hayo, ambapo alisema afya yale imeimarika hasa baada ya kuonyesha uwezo wa kushiriki matembezi hayo ya kilometa tano mwanzo hadi mwisho
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amepumzika na viongozi wenzake baada ya kuwasili kwenye bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya baada ya matembezi hayo
 Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda akisalimiawananchi baada ya matembezi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia mwishoni mwa matembezi hayo
 Mangula akisalimia mwishoni mwa matembezi hayo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akihitimisha matembezi kwa kuwasilimia wananchi baada ya matembezi hayo. Picha zote na theNkoromo Blog

0 comments:

Post a Comment