Chelsea Clinton, Makamu Mwenyekiti wa Clinton Foundation,  na ambaye 
aliongoza majadiliano hayo  akiwatambulisha wanajopo, kutoka kushoto ni 
 Bw. John Heminway, Balozi Tuvako Manongi,    kati kati ni Chelsea  Bint
 wa Rais Bill na Hilary Clinton,  kulia kwa Chelsea ni   Bw. Bryan 
Christy na  anayefuatia  ni   Bw. Josh Ginsberg kutoka Wildlife 
Conservation Society. Heminway na Christy ni waandishi na watunga filamu
 na kwa pamoja wametengeneza filamu ijulikanayo kama  "The Battle for Elephants". Filamu   hiyo  itaonyeshwa  February 27 kupitia  Channel ya National Geograpy. 
 Hapana shaka kwamba Hatari ya kutoweka kwa tembo barani afrika,  ni 
jambo  linalowagusa wengi, washiriki wa majadiliano hayo walitumia fursa
 hiyo kujifunza siyo tu hatari ya kutoweka kwa  mnyama  huyo, lakini pia
 uzuri na sifa zake, na namna gani wanaweza kuchangia  kuhakikisha 
 hatoweki kabisa
 Wadau wa mjadala wakiwa ukumbini
 Waandishi wa habari walikuwepo kwa wingi
Washiriki wakiwa ukumbini
0 comments:
Post a Comment