BENK YA WATU WA ZANZIBAR PBZ YAIBUKA KIDEDEA MWAJIRI BORA KATIKA USHIRIKISHWAJI NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI ZAFICOW

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZAFICAW, Rihii Haji Ali (kushoto), akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Juma Ameir Khafidh cha Mwajiri Bora Katika Ushirikiano na ZAFICOW kwa mwaka 2017. wakati wa hafla ya Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZAFICAW , Rihii Haji Ali (kushoto), akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh cha Mwajiri Bora Katika Ushirikiano na ZAFICOW, wakati wa hafla ya Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
 Viongozi wa PBZ na wa ZAFICOW wakiimbi wimbo wa ushirikiano wa Wafanyakazi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti zilizofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar. 
Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar wakiimbi wimbo wa Wafanyakazi wa Mshikamano wakati wa mkutano wao na Mwenyekiti wa ZAFICOW wakati wa hafla ya bonaza la Michezo lililowashirikisha Wafanyakazi wa PBZ, 
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Rihii Haji Ali ((kushoto)) akitzungumza wakati wa mkutano huo na wafanyakazi wa PBZ kujuwa wajibu wao katika kazi na kuwataka kujiunga na Chama hicho kwa faida yao na maslahi kwa muajiri wao.Pia alikabidhi Kadi kwa Wanachama wapya ya PBZ 10 waliojiunga na kuwakabidhi Kadi za Uwanachama. 
Watendaji wa PBZ wakifuatilia mkutano huo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar Bi Rihii Haji Ali alipokuwa akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa Tamasha la Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Wafanyakazi wa PBZ wakifuatilia mkutano huo na Uongozi wa PBZ na ZAFICOW uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW. Suleiman Abdi (kulia), baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh (kushoto) akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Ndg. Bakari Hussein, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh (wa pili kushoto) akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Fatima Ali Denge, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh (wa pili  kushoto) akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Mkunga Mohammed Saleh, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Mtendajio wa Benki ya Watu wa Zanzibar  Juma Ameir Khafidh akimkabidhi zawada ya fedha shilingi miliono moja kwa kuibuka Mfanyakazi Bora wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa mwaka 2017  Ndg. Juma Ameir Makame (kulia) akishuhudia Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOW) Bi. Rihii Haji Ali hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mfanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg.Haji Masoud, akikisoma Cheti cha Mwajiri Bora Katika Ushirikishwaji katika Chama  cha Wafanyakazi cha ZAFICOW, wakati wa kukabidhi na Uongozi wa ZAFICOW.  
Afisa Muandamizi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Ndg. Anasi Rashid akizungumza na kutowa maelekezo wakati wa Mkutano huo wa Wafanyakazi na Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar Wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOW)  
Mkurugenzi Rasilimali Watu PBZ Ndg. Mohammed Omar (kulia) akimkabidhi zawadi maalum iliyotolewa na Wafanyakazi wa PBZ kwa Boss wao wakati wa Mkutano huo na Wafanyakazi wa PBZ Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Juma Ameir Khafidh akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wakati wa mkutano huo ulioambatana na michezo mbalimbali iliowashirikishwa Wafanyakazi kujumuika pamoja na kubadilishana mawazo Bonaza hilo limefanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambani.Mkoa wa Kusini Unguja.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Khafidh akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na Wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar.


Wafanyakazi wa PBZ wakipata viburudisho ya maji ya madafu baada ya mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.

Imeandaliwa na Othmanmapara.blog.
Zanzinews.com
othmanmaulid@gmail.com


Mobile.0777424152.

POLISI WAPONGEZA VIWANGO VYA MAFUNZO YA KAMPUNI YA ULINZI DAR ES SALAAM

OCD Jiliyo Simba alikuwa mgeni rasmi katika gwaride la kufuzu mafunzo ya maofisa 75 ambao wamekamilisha mafunzo ya msingi ya ulinzi katika sherehe  zilizofanyika siku ya jumamosi tarehe 29, Julai 2017 katika kituo cha mafunzo cha SGA kilichopo Mbezi Beach. 

Maofisa 75 tu ndio waliofuzu mafunzo kati ya 179 ambao walikuwa wanapatiwa mafunzo, jambo linaloonyesha viwango vya juu vya mafunzo ambapo waliobakia wataendelea na mafunzo. 


Vilevile OCD Simba  alikagua vifaa ya kampuni ikiwemo magari ya dharura, magari ya zima moto na chumba cha mfumo wa kuongoza mawasiliano. Alifurahishwa na uwekezaji uliowekwa na kampuni hiyo na udhibiti ambao uko katika utendaji kazi wao, hasa mfumo wa kufuatilia.

Maneja Rasilimali watu wa  (HRM) Ebenezer Kaale, alieleza kuwa mafunzo hayo yalikuwa yanajumuisha vitengo vingi wakiwemo huduma kwa wateja, zima moto, huduma ya kwanza, misingi ya haki za binadamu miongoni mwa vitengo vingi vya muhimu vya kiulinzi. 

“Tunaamini kwamba tumewapatia mafunzo ya msingi ya ulinzi kuweza kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi”, alisema. 

Kabla ya kuajiri,  mchujo na uchunguzi wa kina wa maombi yote. Alama za vidole huchukuliwa kwaajili ya kukagua taarifa za makosa kwa maofisa wa Wizara ya  Mambo ya Ndani huku uchunguzi wa kidaktari hufanyika kwaajili ya kukagua uwezo na stamina kabla ya kuanza mafunzo. 

Wakati wa sherehe, wanafunzi waliofanya vizuri walizawadiwa na kupongezwa na mgeni rasmi ambapo waliopongezwa ni walinzi wawili ambao waliweza kuzuia wezi wa mali za wateja wao wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao. 
Ni utamadumi wa kampuni hii ya ulinzi kutambua utendaji wa kiwango cha juu, vyeti na fedha taslimu viliyolewa wakati wa gwaride kuwahamasisha wengine.   
Vilevile alikuwepo RCO SSP wa Kinondoni John Malulu, ambaye alikuwa OCD wa Kawe. Mr Malulu aliipongeza kampuni ya ulinzi ya SGA kwa ushirikaiano iliyokuwa ikitoa wakati akiwa kiongozi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kawe, kwa kusema kwamba ushirikiano wao ulifanya kazi ya upolisi kuwa nyepesi.

Alibainisha kwamba SGA ilitoa magari kwaajili ya doria siku za mwisho wa wiki na siku za sikukuu na kusaidia polisi katika kufanya ukarabati baadhi ya magari yake. 
“SGA ilikuwa ya kwanza kuitika wateja wao na majirani zake na hiyo ilisaidia kupunguza kiwango cha uhalifu. Ninatarajia msaada na ushirikiano wenu katika nafasi yangu mpya.” Aliongeza. 

Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya SGA bwana Eric Sambu, amesema kwamba kampuni hii ni kubwa kuliko zote hapa Tanzania, na inatilia mkazo katika mafunzo kuwapa uwezo wafanyakazi wao kuweza kutekeleza majukumu yao, ili kuweza kufikia na kuzidi matarajio ya wateja wao. 
“mafunzo kwetu mi kiungo muhimu katika mafanikio yetu na tunatilia mkazo kila aina ya wafanyakazi nchini.”, aliongeza.
Walihitimisha jana mafunzo mengine kwaajili ya timu ya ukaguzi wa fedha ya ndani kwajili ya ISO 9001: 2015, kuhusu Udhibiti wa Ubora, ambayo kampuni hii ithibitishwa tangu 2001. 
Kampuni ya ulinzi ya SGA inatoa huduma ya ulinzi, kusafirisha fedha, ulinzi kwa njia ya mitambo ya kielektroniki, huduma ya muito kwa alarm, huduma ya kufuatilia vyombo vya moto, usafirishaji wa mizigo pamoja na kazi zingine.
Inaendesha pia shughuli zake nchi nzima na ina wafanyakazi wapatao 5,000 na wateja kutoka katika kila sekta ya uchumi. 
Baadhi ya viongozi wakisikiliza

Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi Joakim Sabana akizungumza kwenye hafla hiyo.

Baadhi ya viongozi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, wakiimba wimbo wa Taifa

Baadhi ya viongozi wakitambulishwa.

Askari wa kampuni hiyo wakijiweka tayari kabla ya ukaguzi wa gwaride.

WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI ITUNGI KYELA MKOANI MBEYAWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye badari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chumba cha kulala cha mabaharia wa moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha mitambo ya moja ya meli mbili alizozizindua katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na kujengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wialyani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa

UFUNGUZI WA TAWI JIPYA LA BENKI YA CRDB, CHAKE CHAKE, PEMBA