MHANDISI MALUMA MGENI RASMI MAHAFALI YA TISA, 2017 YA CHUO KIKUU CHA ST. JOSEPH

Mgani Rasmi, Mhandisi Askofu wa Kanisa la Katholiki Jimbo la Njombe  Rev. Alfred Maluma (wa nne kulia) akiwa na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa uliokuwa ukiendelea kabla ya kuanza Mahafali hayo  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 
 Mhandisi, Safiel Chambua
 Mhandisi, Safiel Chambua    pichani akiwa amepozi na mama yake mzazi
  Mhandisi, Safiel Chambua


Mhandisi, Safiel Chambua akiwa na marafiki zake kabla ya kuanza Mahafali hayo yaliyofanyika leo Dar es Salaam April 25, 2017


Bendi ya Matarumbeta ikitumbuiza Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo kikuu cha ST, Joseph Dar es Salaam leo.

Mhandisi, Safiel Chambua (wa pili kulia) akivalia kofia na mwenzake wakati walipokuwa wakila kiapo
Mama mzazi wa Mhandisi, Safiel Chambua, Philipina Chambua (kulia) akimpongeza mwanaye baada ya Mahafali hayo kumalizika Dar es Salaam leo na Tafrija inatarajiwa kufanyika jioni  hii Katika Ukumbi wa Wilivina Hall iyopo eneo la Chuo cha ST. Joseph Magari Saba, Mbezi. anaye shuhudia katikati ni Baba wa Mhandisi, Wilfred Mchome ambaye ni msaafu wa Jeshi la  Polisi 
 Mstaafu wa Jeshi la Polisi,  Wilfred Mchome (wa pili kulia) akimpongeza Mhandisi,   Safiel Chambua  baada ya Mahafali hayo kumalizika na kulia ni mama wa Mhandisi huyo,  Philipina Chambua
Mhandisi,   Safiel Chambua katika picha ya pamoja na wazazi wake mara baada ya kumalizika Mahafali hayo
Mhandisi,   Safiel Chambua akitoka Ukumbini na wazazi wake baada ya kumalizika Mahafali hayo yaliyofanyika katika Ukumbi uliyopo jingo la  Ubungo Plaza Dar es Salaam 

Mhandisi,   Safiel Chambua katika pozi na wazazi wake baada ya kufika nyumbani kwao eneo la Njeteni Mji Mpya, Kata ya Msigani  Mtaa wa Yusufu
Mhandisi,   Safiel Chambua katika pozi na wazazi  na wadogo zake





MNUSO WA HARUSI YA JOHN FOCUS NA BERNADETHA MUNISI JIJINI DAR ES SALAAM


Bwana harusi, John Focus Lyimo akimlisha ndafu mkewe kwenye hafla ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni kabla ya hafla hiyo.

Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akimlisha keki mumewe John Focus Lyimo kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni.

Bwana harusi, John Focus Lyimo (katikati) akiandaa ndafu maalum kwa ajili ya kumlisha mkewe ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani mara baada ya ndoa yao. Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi pamoja na wapambe wao wakiwa kwenye hafla hiyo.

Bwana harusi, John Focus Lyimo (wa pili kushoto) akimtambulisha mkewe Bi. Bernadetha Munishi (wa pili kulia) kwa wageni waalikwa kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Waliokaa ni wapambe wa maharusi.

Dada na mashemeji wa bwana harusi...

Bwana harusi, John Focus Lyimo (kushoto) akipita meza hadi meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam.

Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akipita meza kwa meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam.

Maharusi wakiwaongoza wageni waalikwa kwenye maakuli...

Wanajumuiya wenzake na bwana harusi, John Focus Lyimo kutoka Temboni wakiongozwa na Mr&Mrs Msafiri wakishiriki katika hafla hiyo.

Kulia ni MC Leopold Sondoka (mwenye kipaza sauti) akitoa maelekezo kwa Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi kwenye hafla hiyo.

Wazazi wa Bwana harusi wakiongozwa na mwakilisha wa Baba ndg, Pius Elias (kushoto) wakizungumza machache kwenye hafla hiyo.

Wazazi na ndugu wa bibi harusi wakipata picha ya ukumbusho.

Familia ya bwana harusi ikiongozwa na mwakilisha wa baba ndugu, Pius Elias wakigonganisha glasi kwa furaha

Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi wakionesha furaha yao kwa kugonga chiaz...

Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya harusi hiyo wakigonga chiaz kwa furaha kubwa baada ya kufanikisha shughuli hiyo. Kutoka kushoto ni Mrs. Machonchoryo na Mrs Oscar Munishi.

Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi wakiwalisha vipande vya ndafu 'mades' wao kama ishara ya kuwashukuru.

Wanakamati wakinyanyua keki waliopewa na maharusi kama shukrani kwa kujitoa na kufanikisha hafla hiyo...

Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi (kushoto) wakimkabidhi keki ya asante Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia).

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia) akiwatambulisha wajumbe mbalimbali wa kamati yake.

Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi

MWENYEKITI U.W.T MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA DINI YA KIISLAMU TAMBAZA DAR ES SALAAM JANA

 Mkuu wa Idara ya Biashara na Mlezi wa Wanafunzi wa Sekondari ya Tambaza, Abdul aziz Said  akizungumza na Wazazi  na wahitimu wa shule hiyo wakati wa Mahafali ya  Elimu ya Dini ya kiislam ya Sekondari ya kidato cha sita katika hafla iliyofanyika  Shule hapo Dar es Salaam jana. kulia ni Amiri wa Daawah Msikiti wa Tambaza, Sayed Qadry. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog.
 Mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Maulidi Kassanga akisheherehesha kwa kusoma tenzi katika Mahafali hayo Dar es Salaam jana
 Wahitimu wakiwa katika utulivu wakisikiliza kwa umakini
 Wazazi na ndugu wakifatilia kilichokuwa kikiendelea ukumbini hapo
 Baadhi ya Wanafunzi hao

 Naib Imamu Msikiti wa Maamur, Haroub Khamis (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya Mahafali ya Dini ya kiislam ya Sekondari ya kidato cha sita yaliyofanyika  Shule hapo Dar es Salaam jana ambapo wanafuzi hao wanajiandaa kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha Sita
 Wanafunzi
 Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (U.W.T) Upanga Magharibi, Hajati. Joha Simba (mwenye mtandio mweusi kichwani) akifatilia kwa umakini na wakwanza kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo, Zuhura Gajo
  Mwalimu , Zuhura Gajo akipokea risala kutoka kwa muhitimu, Juma Kassim baada ya kuisoma na kukabidhiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (U.W.T) Upanga Magharibi, Hajati. Joha Simba (kulia)
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (U.W.T) Upanga Magharibi, Hajati. Joha Simba (kulia) akimkabidhi cheti mwanafunzi, Tausi Mohammed wakati wa hafla ya Mahafali ya Dini ya kiislam ya Sekondari ya kidato cha sita yaliyofanyika  Shule hapo Dar es Salaam jana ambapo wanafuzi hao wanajiandaa kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha Sita

 Wanafunzi hao wakiomba Dua wakati walipokuwa wakimaliza mahafali hayo Dar es Salaam jana

 Amiri wa Daawah Msikiti wa Tambaza, Sayed Qadry (kulia) akizungumza na Wazazi na wanafunzi wakati wa Mahafali ya Dini ya Kiislamu katika Shule ya Sekondari ya Tambaza yaliyofanyika Dar es Salaam jana, kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Biashara na Mlezi wa Wanafunzi wa Sekondari hiyo, Abdul aziz Said
Amiri wa Daawah Msikiti wa Tambaza, Sayed Qadry (kulia) akimkabidhi cheti, Rajab Kassim wakati wa hafla ya Mahafali ya Dini ya kiislam ya Sekondari ya kidato cha sita yaliyofanyika  Shuleni hapo Dar es Salaam jana ambapo wanafuzi hao wanajiandaa kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha Sita
Rajab Kassim (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na marafiki zake mara baada ya kumalizika mahafali hayo Dar es Salaam jana
Rajab Kassim, (wa pili kushoto) wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kumalizika mahafali hayo jana