Duru mbalimbali za kijeshi za Sudan zimekiri kuwa wanajeshi kadhaa wa nchi hiyo wameuawa nchini Yemen.
Televisheni ya al Mayadeen ya
nchini Lebanon imezinukuu duru za jeshi la Sudan zinazohusika na vita
vya Yemen zikikiri kuwa wanajeshi watano wa nchi hiyo wameuawaa katika
mapigano na jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, afisa mmoja
wa kijeshi wa Sudan ni miongoni mwa wanajeshi waliouawa huko Yemen.
Wanajeshi wengine 22 wa Sudan wamejeruhiwa.
Mwezi Februari 2016, Saudi Arabia
ilitumbukiza dola bilioni moja katika Benki Kuu ya Sudan na kufanikiwa
kubadilisha msimamo wa Rais Omar al Bashir aliyekubali kushirikiana na
Saudi Arabia katika uvamizi na mauaji ya raia wa Yemen. Hata hivyo fedha
hizo ni kama rehani na amana, wakati wowote Saudia itakapozihitajia,
lazima Sudan izirejeshe. Imechukuliwa hatua hiyo ili kumbana Rais Omar
al Bashir asibadilishe msimamo wake.
Vile vile Saudi Arabia imewekeza katika
miradi ya maji safi nchini Sudan katika hatua nyingine inayoonekana ni
kuwapa hongo Wasudan.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa, mgogoro
wa Yemen ambao ulishadidi kutokana na uvamizi wa Saudi Arabia mwaka
2015, umeshapelekea maelfu ya raia wa kawaida kuuawa na miundombinu
kuharibiwa kabisa.
0 comments:
Post a Comment