Saturday, January 12, 2013

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ZILIVYOFANYIKA LEO

 Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akikagua gwaride lililoandaliwa na vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na JKU, wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwenye Uwanja wa Aaman mjini Zanzibar
 Dk. Shein akipungia mkono vikundi mbalimbali vilivyokuwa vikipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho hayo. Kushoto ni Rais wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete
 Makamu wa Rais, Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour baada ya kuwasili kwenye sherehe hizo
 Dk. Bilal akimsalimia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad. Katikati ni Dk. Salmin Amour
 Dk. Bilal akiwa na Maali Seif na viongozi wengine jukwaa kuu
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mama Mwanamwema Shein na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa kwenye sherehe hizo.
 Waziri Kiongozi Mstaafu,  Shamsi Vuai Nahodha akiwa kwenye sherehe hizo.
 Waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye sherehe hizo.
 Wananchi wakiwa kwenye sherehe hizo
 Wananchi wakiingia Uwanjani kwa mandamano maalum
 Kikosi cha JWTZ kikipita mbele ya Jukwaa kuu kwa heshima
 Kikosi cha Magereza wakipita mbele ya Jukwaa kwa heshima
 Kikosi cha wanamaji kikipita mbele ya Jukwaa kwa heshima
 Kikosi cha Bendera
 Dk Shein akihutubia kilele cha sherehe hizo. Picha na Wapigapicha Maalum

Sunday, December 30, 2012

ISAKWISA MWAIFUGE AOA

 Rais wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka wafuasi wake rasmi na kuvunja katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.
 Maharusi, wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya keki.
 Hapa ilikuwa ni muda wa Kwaito..........
 Sehemu ya wageni waalikwa.....
 Wadau kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya Sufiaimafoto.
 Baadhi ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi, wakipozi kwa picha, baada ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya Keki.
 Sehemu ya wageni waalikwa,..
Salum Mkambala, akisebeneka kwa staili yake wakati akielekea kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wa Chanel Ten.

Thursday, December 27, 2012

TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600,MWANZA

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania
 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600. (PICHA NA MDAU BALTAZAR MASHAKA)

 Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo.
 Diwani wa Kata ya Mkuyuni, ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula , Lugo Fasheni akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti  unaotekelezwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL ), jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. TBL tayari imesaidia kupanda miti 2600 jijini Mwanza.

  Afisa Misitu Jiji la Mwanza, Kaombe Phidelis, akitoa taarifa ya hali ya misitu kwa mgeni rasmi , Henry Mongi wa pili kutoka kushoto,katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jana.Wa kwanza ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria TBL, Steven Kilindo .
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegezi na mtumishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakipanda mti kwa pamoja katika shule hiyo, jijini Mwanza juzi. TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600

Monday, December 24, 2012

NAIBU WAZIRI ANGELLA KAIRUKI NA SCHOOLMATE WAKE WA ZANAKI


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angella Kairuki akishow love na my schoolmate wake Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu katika viwanja vya Mnazi hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani.

Friday, December 14, 2012

JK AIPATIA TBL TUZO YA MWAJIRI BORA 2012

Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali  Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto cheti baada y kuwa mmoja wa wafadhiri wa hafla ya kuwazawadia waajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
 Mkurugenzi wa Rasilimali  Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto akishangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete kumkabidhi tuzo ya ushindi wa tatu ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto cheti baada y kuwa mmoja wa wafadhiri wa hafla ya kuwazawadia waajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
 Wanyoto akipita na tuzo mbele ya Rais Kikwete pamoja na Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
                        Reynada Sikira wa TBL, akipokea tuzo nyingine waliyoshinda
                            Meza waliyokuwa wamekaa baadhi ya wafanyakazi wa TBL
                                                           Wanyoto (kulia) akiwa na furaha

HAFLA YA WAZIRI DK. MGIMWA KUKABIDHI TUZO WAFANYAKAZI BORA

 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (kushoto)  akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa (kulia) . Tafrija fupi ilifanyika jana mjini Dar es salaam kufuatia kuchaguliwa kwake mwezi Mei mwaka huu kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2012.
 Mkuu wa Mfuko wa Mikopo wa Hazina kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali , Wizara ya Fedha Christina Ngonyani (kushoto)  akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ilifanyika jana mjini Dar es salaam kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2012.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto)  akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa Wizara hiyo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ya kuwazawadia wafanyakazi bora ilifanyika jana mjini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.

 Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa (katikati) akiwapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walichaguliwa mwezi Mei mwaka huu kuwa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012. Tafrija fupi ya kuwazawadia wafanyakazi bora ilifanyika jana mjini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa , Katibu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah wakishirikiana na viongozi wa TUGHE na wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa tafrija fupi jana ya kuwapongeza wafanyakazi bora  wa mwaka huu. Picha zote na GCU- HAZINA

MKUTANO WA SITA WA MENEJIMENTI YA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Ndg. Justine Mwandu akifungua mkutano wa Sita wa Mameneja wa shirika hilo katika hoteli ya Sea Scape iliyopo maeneo ya Mbezi, Dar es Salaam tarehe 3 Desemba 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bima za Maisha, Bi. Rose Lawa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Anne Mbughuni. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bima za Mali na Ajali, Ndg Ndugu Kura Kalema.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mwandu (kushoto) akiwakaribisha wajumbe katika mkutano. Anayesalimiana nae ni meneja wa bima tawi la Songea Ndugu Moses Senje akifuatiwa na meneja mwenzake tawi la Tanga Ndugu Romanus Hokororo na mwisho meneja wa Iringa Ndg Ally Mohammed.
Kutoka kulia ni Bw. Henry Machoke, Mkurugenzi wa Masoko, akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa NIC, Elisante Maleko, na Meneja wa tawi la Ubungo, Segeja Mabula katika mkutano huo.
akurugenzi pamoja na Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano.