ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN NCHINI INDIA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii wa India Shri Ghulam Nabi Azad, alipowasili katika hoteli ya Oberoi Mjini New Delhi alipofikia Rais na Ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini India
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa India Shri Ghulam Nabi Azad, alipowasili katika hoteli ya Oberoi Mjini New Delhi alipofikia Rais na Ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini India
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake wakizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa India  Shri Ghulam Nabi Azad,na Viongozi aliofuatana nao walipofika katika hoteli ya Oberoi Mjini New Delhi alipofikia Rais na Ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini India
  Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini India wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao jana katika ukumbi wa jengo la Hotel ya Ashok Mjini New Delhi,akiwa katika ziara nchini India ya siku tisa katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo
 Viongozi wa Ujumbe wa Rais na Vingozi wa Watanzania Nchini India  pamoja na wanafunzi wanaosoma  kupata fani mbali mbali nchini India,wakimasikiliza  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa nasaha zake wakati walipokutana jana katika ukumbi wa Hotel ya Ashok Mjini Nwe Delhi India
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Watanzania Wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbali mbali nchini India, jana katika ukumbi wa Hotel the Ashok mjini New Delhi,akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na mashirikiano na nchi hiyo,(kulia wa kwanza) Waziri wa Uwezeshaji,Vijana wanawake na Watoto,Bi Zainab Omar Mohamed,Mama Mwanamwema Shein,na (kushoto) Balozi wa Tanzania nchini India John W.H.Kijazi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee na Balozi wa Tanzania nchini India John W.H.Kijazi, ni miongoni mwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara nchini India, pichani wakimsikiliza Rais wakati alipozungumza na watanzania katika ukumbi wa The Ashok Hotel Mjini New Delhi jana
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa picha ya pamoja na Watanzania wanaosoma nchini India baada ya mazungumzo ya  pamoja nao jana katika ukumbi wa The Ashok Hotel Mjini New Delhi akiwa katika ziara ya Kiserikali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa picha ya pamoja na Watoto baada ya mazungumzo ya  pamoja na Watanzania  jana katika ukumbi wa The Ashok Hotel Mjini New Delhi India akiwa katika ziara ya Kiserikali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,(kulia) wakiwa picha ya pamoja na Makamo wa Rais wa India Mohammed Ansari na Mkewe Salma Ansari,walipoalikwa chakula cha usiku jana katika ukumbi wa Hayderabad House, Mjini New Delhi akiwa katika ziara ya Kiserikali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,  wakisalimiana na Viongozi wa Serikali ya India wakati wa hafla ya chakula cha usiku jana kilichoandaliwa na  Makamo wa Rais wa India Mohammed Ansari na Mkewe Salma Ansari,katika ukumbi wa Hayderabad House, Mjini New Delhi akiwa katika ziara ya Kiserikali.
Makamo wa Rais wa India Mohammed Ansari na Mkewe Salma Ansari, wakisalimiana na ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipowatambulisha jana wakati wa chakula cha usiku katika ukumbi wa Hayderabad House, Mjini New Delhi  katika ziara ya Kiserikali Nchini India. (Picha zote na Ramadhan Othman wa Ikulu).

0 comments:

Post a Comment