Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya 
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili 
uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru 
leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis 
Mwamunyange.
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya 
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 
21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo 
uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya 
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya 
Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 
ya Uhuru.
Sehemu
 ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa 
ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo
 leo jijini Dar es salaam.
Mke
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma 
Kikwete  akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za 
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.
 Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.
Rais
 Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi
 Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na 
Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu  la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa 
haraka.
Baadhi
 ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa 
wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wananchi
 wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 
52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Vijana
 wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya 
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es 
salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, 
Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”
Vijana
 wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana 
mfano wa mnyama aina ya simba kuashiria utalii katika hifadhi  za 
wanyama za Tanzania.
Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.
Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya 
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa
 maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya
 kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini  Mzee 
Nelson Rolihlahla Mandela Madiba  aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya 
Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa  watanzania na
 kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo 
madarakani.
Rais
 wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi 
Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa 
na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa 
Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Raia
 wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara 
wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari 
(MAELEZO) leo.
Rais
 Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis 
Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na 
Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Mwenyekiti
 wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa 
viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya 
Uhuru.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
0 comments:
Post a Comment