KINANA AZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO DIMANI, ZANZIBAR LEO

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni zake katika jimbo la Dimani mkoa wa mjini magharibi kisiwani Unguja na kukishangaa chama Cha wananchi  (CUF) kwa kushindwa kutanua wigo wa demokrasia ndani ya chama hicho na kuendelea kumshikilia mgombea mmoja wa urais Zanzibar  wa kudumu miaka kwa miaka .

Kimesema wananchi wataendelea kukichagua chama hicho tawala kwa sababu ya kufuata  misingi bora ya  demokrasia, misimamo thabiti, sera endelevu  na utamaduni wake wa kubadilisha wagombea .

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana (pichani juu), wakati akizindua kampeni za CCM uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani,  zilizofanyika katika eneo la Maungani nje kidogo ya mji wa Unguja.

Kanali Kinana alisema CCM itaendelea kuchaguliwa na wanqnchi kwasababu kinatimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi, kutikiza matakwa ya kisera na kushughulikia matatizo na shida za wananchi.

"Demokrasia ndani ya chama chetu ni ni ya aina yake na kwamba  kukubalika kwetu mbekw ya wananchi nikutokana na  misimamo yetu inayotetea maslahi ya umma na vile vile demokrasia ndani ya CCM haifanani na vyama vingine ", Alisema Kinana.

Alisema chama hicho kina umoja imara, hazuiwi mwanachama kuwania nafasi ya uongozi na kwamba hakina sifa ya kuwa na wagombea wa kudumu kama kilivyo chama  cha CUF  ambacho tokea kilipozishwa mwaka 1992 hadi sasa Katibu mkuu na mgombea urais ni huyo huyo  Maalim Seif Sharif Hamad

Pia Katibu  mkuu huyo alisema kushiriki kwa wagombea takriban 25 ndsni ya CCM waliowania nafasi ya ubunge jimbo la Dimani na kupatikana mmoja huku akiungwa mkono na wenzake ni kieelezo tosha  kuwa ndani ya chama hicho  kuna umoja imara na demokrasia ya kweli.

Alieleza kuwa vikao vya CCM vya Nec na kamati kuu   vimeketi kujafili hatimaye kupitisha jina la mgombea aliyeshinda kura za maoni huku chama cha CUF kikiwa kimya na bila kufanyika vikao vya kikatiba.

Akizumgumzia kupwaya kwa dhana na misingi yq demokrasia ndani ya CUF, Kinana alikipinda chama hicho na kusema kuwa hivi sasa chama hicho kina wenyeviti watatu, mmoja akiwa wa muda, mwingine wa mpito na aliyebaki ni wa zamani

"Kuna mgombea mmoja hapa Zanzibar ameanza kugombea urais tokea akiwa na miaka 30 na sasa ana miaka 80, toka akiwa bado kijana mbichi  sasa amekuwa  kikongwe na kupinda mgongo ila bado ana tamaa ya kuwania urais" Alisema Kinana.

Aidha Kinana aliwashangaa wanachama wa CUF ambao wanakubali kudanganywa kirahisi kila siku na kuaminishwa iko siku mgombea wao wa urais sliyeshindwa uchaguzi atatangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Rais wa Zanzibar.

"Tuliambiwa hapa  uchaguzi mkuu wa Zanzibar utafutwa, watakuja watu  toka UN , mara tukaelezwa wangekuja   jumuiya ya ulaya, wakaambiwa washone nguo mpya kusherehekea ushindi huku siku zikitaradadi hakuna kinachotokea "Alieleza Kinana.

Hata hivyo Kinana alisema chama cha CUF viongozi wake hawana  uwezo wowote wa kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendelwo kwa maelezo kuwa walibahatika kuingia katika seikali ya umoja wa kitaifa na kushindwa kufanya lolote.

"Kama ni mkate CUF walipata nusu na CCM  nusu, wakashika Wizara makini za Biashara na Viwanda, Katiba na Sheria, Haabari na Utamaduni, mawasiliano na miundombinu lakini kutokana na wao kuwa udhaifu, hawakumudu  hata kujenga kiwanda kidogo"Alisisitiza

Katibu Mkuu huyo wa CCM  aliwaomba wananchi wa Dimani kumchagua mgombea ubunge aliyesimamishwa kwa tiketi ya CCM Juma Ali Juma kwasababu ni makini, mchapakazi na mwepesi wa kuwatumikia wananchi.

Akihutubia Katika mkutamo hup wa uzinduzi wa kampeni, mjumbe wa kamati kuu ya ccm Balozi Seif Ali Idd aliwaeleza wananchi wa jimbo la Dimani kuwa si sifa ya wagombea wa CUF kuwatumikia wananchi na mfano mzuri ni katika majimbo ya pemba.

Balozi Seif ambaye ni makamu wa pili wa Rais Zanzibar, alisema viongozi wa chama hicho hawana uzoefu wala historia ya kuwatumikia wananchi katika majimbo yote walibahatika kushinda "Alieleza Balozi Seif.

"Sifa ya kuwatumikia wananchi ni ya ccm na viongozi wake,yatazameni majimbo ya Pemba, Mji Mkongwe na Nungwi, yako taaban kwasababu wawakikshi  waliochaguliwa hawana uwezo na dhamira ya kuwatumikia watu "alieleza Balozi Seif.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa mwemvuli wa ccm Juma Ali Juma alisema amejipanga kuwawakilisha wananchi ipasavyo,  kuwatumikia, kushirikiana nao na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya ccm inatekelezwa hatua kwa hatua.

Katika mkutano huo wa uzinduzi  umehudhuriwa na mke wa makamu wa pili wa Rais Mama Asha Suleiman Idd,  Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa Itikadi na Uenezi Hamperey Polepole na Katibu wa Oganaizeshaeni Dk Mohammed Seif Katibu , Spika Mstaafu wa baraza la wawwkilishi zanzibar Pandu Amir Kificho na mwenyeliti wa ccm mkoa wa Mgjaribu Yusuf Mohammed Yusuf. 

0 comments:

Post a Comment