UJUMBE WA KINAMAMA KUTOKA VYAMA VYA SIASA VYA MALAWI WAKUTANA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA( UWT), TAIFA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba (kushoto) akizungumza  wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu, katika ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa (kushoto), na Ujumbe wa Kinamama kutoka vyama vya siasa nchini Malawi (kulia), uliotembelea Makao Makuu ya UWT Taifa, jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo kutoka Malawi, upo nchini Tanzania, kwa mwaliko wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zifutazo ni picha mbalimbali kuhusu tukio hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Zarina Madabida (kulia) akifafanua jambo, wakati wa kikao hicho. Kushoto pia ni Wajumbe wa Kamati hiyo ya Utekelezaji.

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Unoja wa Wanawake wa Tanzania UWT, wakiwa na Kinamama kutoka vyama vya siasa vya Malawi, wakati wa kikao hicho

0 comments:

Post a Comment