JK AONGOZA KIKAO CHA NEC LEO MJINI DODOMA, NI KIKAO CHAKE CHA MWISHO, WAJUMBE WAPITISHA KWA KISHONDO JINA LA RAIS DK. MAGUFULI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuongoza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuingia ukumbini, kwa ajili ya kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) leo katika ukumbi wa Sekretarieti uliopo katika Jengola White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo. Wanaofuata ni Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa , Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa ,Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja, ya kupokea jina la Rais Dk. Magufuli ili kuliafiki au kulikataa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa awamu ya tano kufuatia Mwenyekiti wa sasa atakapostaafu na kumwachia kijiti cha uongozi huo wa Chama katika mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika kesho katika Ukumbi wa Dodoma Convetion.
ZIFUATAZO NI PICHA ZA WAJUMBE KATIKA  MATIKO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO HUO>>>PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

0 comments:

Post a Comment