MKUTANO WA MWAKA WA TANAPA NA WAHARIRI NA WANAHABARI WAANDAMIZI WAMALIZIKA LEO MJINI MOROGORO

  Mmoja wa Washiriki wa Mkutano huo, Deo Mushi, akisoma maazimio baada ya mkutano wa Wahariri na waandishi wa habari waandamizi, uliofanyika leo katika ukumbi wa VETA, mjini Morogoro. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Pascal Shelukindo, TANAPA ndiyo walioandaa mkutano huo kwa lengo la kuwajengea uelewa kwa wanataaluma hao wa habari kuhusu shughuli za TANAPA. Baadaye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, alikabidhi vyeti kwa washiriki na kisha kuufunga mkutano huo. Zifuatazo ni picha mbalimbali katika mfululizo wa kukabidhi vyeti hivyo.Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, akifunga mkutano huo baada ya kukabidhi vyeti kwa washiriki. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

0 comments:

Post a Comment