HOTUBA YA MHE. DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE BARAZA LA EID EL FITR, TABORA, TAREHE 9 AGOSTI 2013

Mheshimiwa Mufti wa Tanzania ,
Sheikh Issa bin Shaaban Simba;

Mheshimiwa Fatma Mwassa
Mkuu wa Mkoa wa Tabora;

Viongozi wa Dini na Madhehebu Mbalimbali;

Viongozi wa Mkoa wa Tabora na Mikoa jirani;

Katibu Mkuu wa BAKWATA;

Wajumbe wa Baraza la Ulamaa;

Viongozi Mbalimbali wa BAKWATA;

Wageni Waalikwa;

Ndugu Waumini;

Ndugu Wananchi;

Eid Mubarak!

Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima,  afya njema na kutuwezesha kujumuika hapa siku ya leo kuadhimisha tukio hili  muhimu la kumalizika kwa mfungo  wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Napenda nitumie fursa hii, kutoa shukrani zangu    za   dhati   kwako   Mufti   wa Tanzania , Shekhe Issa bin Shaaban Simba na uongozi mzima wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), kwa heshima mliyonipa, kunialika kuwa mgeni rasmi katika sikukuu hii muhimu.

Aidha niwapongeze wale wote waliojaaliwa kukamilisha ibada hii adhimu, ambayo ni moja ya nguzo kuu katika imani ya dini ya Kiislamu. Kwa wale ambao hawakupata bahati hiyo, tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu awajalie uhai na kuwatunuku fursa hiyo siku zijazo. Rai yangu kwa mlioshiriki ibada hii muhimu ni kwamba; endelezeni mema yote mliyofanya na kuonesha   katika  kipindi chote cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Matendo mema yawe sehemu ya utamaduni wa maisha yetu ya kila siku katika jamii. Naamini kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunatekeleza kwa vitendo mafundisho ya Mtume wetu Mohammad (S.A.W) na kujiwekea fungu jema duniani na akhera.

Ucha Mungu, upole, adabu, upendo, ustahimilivu na mambo yote mema mliyowatendea ndugu, jamaa na majirani zenu katika kipindi chote cha mfungo wa Ramadhani,   yadumu   na   kuwa   kielelezo  na ushahidi wa imani yenu mbele ya wanadamu wenzenu. Kwa mwislamu mwenye imani ya kweli, kuwajali wenye shida, wajane na yatima, ni ibada muhimu kwa maisha yake ya kila siku, hili halikomi baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Endeleeni kujitoa kwa ajili ya wenye shida, salini kwa bidii na kuzingatia mafundisho yote ya Mtume wetu Mohammad (S.A.W) mliyoyapata wakati wa mfungo. Kumbukeni kuwa kumcha Mwenyezi Mungu ni msingi wa  mafanikio  yote  hapa  duniani.   Jamii  ya  watu wacha Mungu ni jamii iliyostaarabika, isiyo na chuki, mifarakano wala ugomvi, zaidi ya hayo; inatii sheria na kuheshimu mamlaka zote zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Mufti wa Tanzania ;
Ndugu Waumini;
Ndugu Wananchi;

0 comments:

Post a Comment