KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA MITANO YA SHULE YA LITTLE TREASURES YAFANA


Hapa ni katika shule ya msingi Little Treasures iliyopo eneo la Bugayambelele katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi,Agosti 13,2016 kumefanyika sherehe ya maadhimisho ya miaka Mitano tangu kuanzishwa shule hiyo Julai mwaka 2011.

Sherehe ya maadhimisho ya miaka mitano ya shule hiyo imefanyika katika eneo la shule hiyo na kuhudhuriwa na wazazi na walezi wa watoto,walimu,wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu.

Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa alisema siku mbili kabla ya kilele cha maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, wanafunzi wa shule hiyo walitembelea Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija,Hospitali ya rufaaa ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto soma <<HAPA>>.

Nchagwa alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi wanne na sasa ina jumla ya wanafunzi 540.
Naye Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic aliwataka wazazi na walezi kuendelea kushirikiana na shule hiyo ili kuhakikisha kuwa watoto wanaosoma katika shule hiyo wanatimiza ndoto zao huku akisisitiza kuwa mazingira ya shule hiyo ni rafiki kwa elimu bora ya wanafunzi.

Aliongeza kuwa ni wajibu wa wazazi na walimu kushirikiana pamoja katika kuwalea watoto hivyo kuwasisitiza wazazi na walezi wa watoto kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao ili wakue katika maadili mema.

Michezo mbalimbali kutoka kwa wanafunzi,wazazi na wafanyakazi wa shule hiyo ilikuwepo katika kunogesha sherehe hiyo.

Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametusogezea picha 60 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa chini
Nje ya geti la shule:Bango likionesha kile kilichokuwa kinaendelea katika shule ya Little Treasures ambayo pindi tu ufikapo lugha ya kawaida zinazotumika ni Kiingereza,Kifaransa na Kiswahili kidogo
Mbele ya jengo la utawala shule ya Little Treasures
Muonekano halisi wa shule ya Little Treasures
Keki maalum kwa ajili ya sherehe ya kuadhimisha miaka mitano ya shule ya msingi Little Treasures yenye wanafunzi zaidi ya 500 na walimu wa kutosha
Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic akiwasalimia wageni mbalimbali waliofika katika sherehe hiyo ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule yake mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi wanne na sasa ina zaidi ya wanafunzi 500 kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga
Wazazi wakiwa eneo la tukio wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akizungumza wakati wa sherehe ya miaka mitano ya shule hiyo.Kushoto ni wanafunzi wa shule hiyo
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Wageni waalikwa na wazazi wakiwa eneo la tukio
Wanafunzi wa darasa la watoto (Baby Class) wakitoa burudani ya wimbo 
Wanafunzi wa shule ya awali daraja la pili (Middle Classa) wakiimba wimbo
Wanafunzi wakiwa eneo la tukio
Wanafunzi wa Middle Class wakitoa burudani ya wimbo
Mmoja wa wanafunzi wa Middle Class akifundisha wazazi waliofika katika sherehe hiyo namna ya kutamka maneno
Tunafuatilia kinachoendela hapa....
Wanafunzi wa shule ya awali daraja la tatu/daraja la mwisho (Pre -Unit) wakiimba wimbo
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiunda umbo la muonekano wa shule yao ya Little Treasures
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiimba wimbo
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiendelea kutoa burudani
Wazazi wakifurahia burudani
Wazazi wakiwa eneo la tukio
Wanafunzi wa darasa la pili  wakitoa burudani
Wanafunzi wa darasa la tatu wakikariri shairi
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akisoma risala ambapo alisema pamoja na shule hiyo kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma kwa kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali,kuwa na mabasi ya kusafirisha wanafunzi hadi majumbani mwao sasa shule hiyo imefanikiwa kujenga bweni kwa ajili ya wanafunzi huku ikiendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa samaki,ng'omben.k
Wazazi wakiwa eneo la tukio
Pamoja na wanafunzi kuonesha michezo mbalimbali wazazi nao hawakuwa nyuma kushiriki katika michezo...Mchezo wa wazazi kukimbiza kuku ulichukua nafasi 
Wanafunzi wakishuhudia wazazi wao wanavyokimbiza kuku
Mshindi wa shindano la kukimbiza kuku akiwa ameshikilia kuku wake
Wanafunzi wa darasa la nne wakiimba na kucheza muziki
Wazazi wakiwa chini ya mti wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Wanafunzi wa darasa la nne wakicheza Ngoma ya asili kutoka kabila la Kikurya
Wanafunzi wa darasa la nne wakionesha vipaji vyao vya kucheza nyimbo za asili
Wazazi wakiwa eneo la tukio
Wanafunzi wa kwaya ya shule wakitoa burudani
Wanafunzi wa darasa la tano wakiimba wimbo wa Kifaransa
Wanafunzi wa darasa la tano wakicheza
Wanafunzi wa darasa la tano wakiendelea kutoa burudani
Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Little Treasures Tilulindwa Sullusi akizungumza katika maadhimisho ya miaka mitano ya shule hiyo.Sullusi aliwataka wazazi kushirikiana na shule hiyo ili kuhakikisha kuwa watoto wanatimiza ndoto zao
Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic akizungumza katika sherehe hiyo ambapo alisema wataendelea kushirikiana na wazazi,jamii inayowazunguka kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki ya elimu katika mazingira rafiki zaidi.
Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic pia alihamasisha wazazi kuwasimamia watoto wao majumbani badala ya kuwaachia walimu pekee
Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic alisema shule yake inaendelea kuibua vipaji vya watoto na kuomba jamii kupeleka watoto wao katika shule hiyo kwani ina mazingira rafiki ya elimu kwa watoto
Washindi wa shindano la kusaka mtoto wa mfalme wa kiume na wa kike wa shule ya Little Treasures (Prince na Princess) wakiwa jukwaani
Prince wa shule ya Little Treasures akipunga mkono kwa wazazi
Wazazi wakiwa eneo la tukio
Tunafuatilia kinachoendelea
Wanafunzi wa darasa la sita wakionesha michezo mbalimbali
Burudani inaendelea
Wanafunzi wa darasa la sita wakionesha michezo yao
Wanafunzi wakiimba na kucheza ngoma
Wafanyakazi wa shule ya Little treasures wakijiandaa na shindano la kuvuta kamba.Shindano hilo lilikuwa kati ya wafanyakazi wa shule hiyo na wazazi wa wanafunzi
Wazazi wakijiandaa kuvuta kamba...ambapo hata hivyo waliibuka washindi
Keki maalum kwa ajili ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule ya Little Treasures
Mzazi na wanafunzi waliozaliwa Agosti 13 wakikata keki kwa ajili ya wanafunzi,wafanyakazi wa Little Treasures,wazazi na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe ya kutimiza miaka mitano ikiwa pia ni sehemu ya kusherehekea siku zao za kuzaliwa
Mzazi,watoto wakilishana keki
Wanafunzi wakilishana keki
Wazazi wa wanafunzi waanzilishi,wanafunzi waanzilishi na wafanyakazi wa shule ya msingi Little Treasures wakilishana keki
Zoezi la kulishana keki linaendelea
Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic akifurahia jambo la wazazi
Baada ya kufungua Shampen.... mzazi anagawa kinywaji kwa wanafunzi
Mzazi akigawa kinywaji meza kuu
Meneja wa shule ya msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akizungumza wakati wa kufunga sherehe hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alisema wanategemea kufungua shule ya sekondari mwaka 2018
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Bofya <<HAPA>> Kuona matukio zaidi ya shule ya Little Treasures

0 comments:

Post a Comment