Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,
Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu
cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya
kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani
akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja
wa Mataifa unaofanyika New York.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi
wa juu wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya kuwasili chuoni hapo. Kulia
kwa Mama ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi
akifuatiwa na Naibu Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ramadhani
Mwinyi, na Ms Janet Mahoney,wa Chuo Kikuu cha Monmouth na kushoto kwa
Mama Salma ni Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu hicho, Bwana Saliba
Sarsar, Makamu Rais wa Chuo cha Monmouth anayeshughulikia mahusiano ya
kimataifa na Mwisho ni Bwana John McLaughlin, kutoka Shirika la
Footprints for Education International la nchini Marekani.
Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth Dr. Paul Brown, akimtembeza Mama Salma
Kikwete maeneo mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu
mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa
katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma
Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein
Mwinyi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama
Salma Kikwete akijadiliana jambo na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu
cha Monmouth baada ya Mama Salma kumkabidhi Jarida litolewalo na Taasisi
ya WAMA .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu
mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa
katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma
Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein
Mwinyi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kitabu kutoka kwa Dk. Edward
Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho
kilitoa zaidi ya vitabu 4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine
wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein
Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John
McLaughlin.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kitabu kutoka kwa Dkt. Edward
Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho
kilitoa zaidi ya vitabu 4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine
wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein
Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John
McLaughlin.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anazungumza na Bwana Kevin Williams,
Mwalimu kutoka shule ya Asbury Park. Shule hiyo ina uhusiano na shule
ya sekondari ya WAMA, iliyoko huko wilayani Rufiji, mkoani Pwani. PICHA NA JOHN LUKUWI WA MAELEZO
MKE WA RAIS, MAMA SALMA KIKWETE ATINGA CHUO KIKUU CHA MONMOUTH NEW JERSEY, MAREKANI
About Bashir Nkoromo
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment