ALIYEWAHI KUWA MKURUGENZI MKUU HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ANATARAJIWA KUZIKWA LEO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI DAR ES SALAAM LEO

 Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiwasili katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ukisindikizwa na wanataaluma jana April 11, 2017 ambapo mwili unatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni leo April 12, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru (kulia) akiangalia mwili wa Marehemu Profesa Maselle ukishushwa toka katika gari maalumu lililokuwa limebeba mwili huo jana, wapili kulia ni Profesa Ayubu Magimba
 Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Ukiwasili katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ambapo taratibu za kutowa heshima za mwisho zilifanyika jana April 11, 2017 na leo April 12, 2017 mwili huo unatarajiwa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
 Wanataaluma mbalimbali wakiwa wanaushusha mwili wa mpendwa wao marehemu Profesa, Samuel Maselle kwa maandalizi ya kutowa heshima za mwisho jana
 Baadhi ya viongozi katika meza Kuu akiwemo Profesa, Ephata Kaaya (wa tatu kushoto) wapilikushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Lawrence Museru na wa kwanza kushoto ni Profesa Ayub Magimba
 Baadhi ya wanafamilia na wana Taaluma wa Muhas
 Kaimu Mkuu wa Skuli ya Tiba, (MUHAS) Dokt, Erasto Mbugi akisoma wasifu wa Marehemu
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akisoma wasifu kwa niaba ya Hospitali ya Taifa na kutowa Rambirambi kwa niaba  ya wafanyakazi wa hospitali hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete akisoma wasifu wa Marehemu Maselle kwa niaba ya Taasisi hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt, Respicious Boniface akisoma wasifu kwa niaba ya Taasisi hiyo na kutowa Rambirambi kwa niaba  ya wafanyakazi wake
 Ndugu wa Marehemu akishukuru kwa wote waliyojitolea kwa hali na mali kushirikiana na familia bega kwa bega kusaidia kuokoa maisha ya ndugu yao na hata mlipo sikia ndugu yetu katutoka hamkutuacha peke yetu na mmekuwa mstari wa mbele kufanikisha shughuli nzima za maandalizi ya kumsindikiza mpendwa wetu Profesa Maselle kuelelea katika nyumba yake ya milele na mmekuwa nasi mwanzo hadi kufikia tulipo fikia. nawashukuruni sana na mungu awabariki
 Sehemu ya wanataaluma mbalimbali
 Baadhi ya wana taaluma wakifatilia kwa umakini yaliyokuwa yakiendelea Chuoni hapo
 Aliyewahi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr. Marina Njelekela akitowa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurungezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Samuel Maselle katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas 
 Waombolezaji wakitowa heshima za mwisho
 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (aliyeshika mwamvuli) akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt, Respicious Boniface akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitaliya Taifa Muhimbili
 Wanataaluma wakiubeba mwili wa marehemu Maselle kuuweka katika gari maalumu tayari kwa kuelekea nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach
Mwili wa Marehemu Maselle ukiingizwa jana katika Gari
khamisimussa77@gmail.com

Posted in

Spread the love

SUDAN YAKIRI KUUAWA WANAJESHI WAKE NCHINI YEMEN

Duru mbalimbali za kijeshi za Sudan zimekiri kuwa wanajeshi kadhaa wa nchi hiyo wameuawa nchini Yemen.
Televisheni ya al Mayadeen ya nchini Lebanon imezinukuu duru za jeshi la Sudan zinazohusika na vita vya Yemen zikikiri kuwa wanajeshi watano wa nchi hiyo wameuawaa katika mapigano na jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, afisa mmoja wa kijeshi wa Sudan ni miongoni mwa wanajeshi waliouawa huko Yemen. Wanajeshi wengine 22 wa Sudan wamejeruhiwa.
Rais Omar al Bashir wa Sudan

Mwezi Februari 2016, Saudi Arabia ilitumbukiza dola bilioni moja katika Benki Kuu ya Sudan na kufanikiwa kubadilisha msimamo wa Rais Omar al Bashir aliyekubali kushirikiana na Saudi Arabia katika uvamizi na mauaji ya raia wa Yemen. Hata hivyo fedha hizo ni kama rehani na amana, wakati wowote Saudia itakapozihitajia, lazima Sudan izirejeshe. Imechukuliwa hatua hiyo ili kumbana Rais Omar al Bashir asibadilishe msimamo wake.
Vile vile Saudi Arabia imewekeza katika miradi ya maji safi nchini Sudan katika hatua nyingine inayoonekana ni kuwapa hongo Wasudan.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa, mgogoro wa Yemen ambao ulishadidi kutokana na uvamizi wa Saudi Arabia mwaka 2015, umeshapelekea maelfu ya raia wa kawaida kuuawa na miundombinu kuharibiwa kabisa.
khamisimussa77@gmail.com

Posted in

Spread the love

BASI LA BORUSSIA DORTMUND LAKABILIWA NA MLIPUKO

Mechi hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Champions League, kati ya Borussia Dortmund na Monaco, ilikuwa ichezwe jana (11.04.2017) katika uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund.
Basi la timu ya Borussia Dortmund limeharibiwa na abiria mmoja kujeruhiwa baada ya milipuko mitatu kutokea karibu na basi hilo lililokuwa njiani kuelekea uwanja wa Signal Iduna Park umbali wa kiasi kilometa kumi ambako mechi ya ligi ya mabingwa, Chamiopns League, ilitarajiwa kuchezwa. Tukio hilo limetokea mwendo wa saa moja usiku saa za Ujerumani.
Msemaji wa jeshi la polisi katika jimbo la North Rhine Westphalia, Gunnar Wortmann, aliliambia shirika la habari la Associated Press, "Basi lilianza safari kutoka hoteli ya timu ya Dortmund wakati milipuko mitatu ilipotokea. Milipuko mitatu ilitokea karibu na basi hilo lilipokuwa njiani kuelekea uwanjani na kwamba mchezaji mmoja amejeruhiwa na dirisha moja kuharibiwa."
Beki wa Dortmund ajeruhiwa
Fußball Bundesliga Borussia Dortmund - FC Ingolstadt 04 Marc Bartra (picture-alliance) Beki wa Dortmund, Marc Bartra
Gazeti la Ujerumani la Bild limeripoti kwamba beki wa Borussia Doetmund Marc Bartra amejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Klabu ya Dortmund imetuma taarifa katika mtandao wa kijamii wa Twitter ikisema mchezaji huyo yuko salama na hakuna kitisho chochote ndani na nje ya uwanja wa Signal Iduna Park.
Mkurugenzi wa klabu ya Dortmund, Hans-Joachim Watzke, alithibitisha kujeruhiwa kwa Bartra, akisema ameumia mkononi na kuwa majeruhi si hatari kwa maisha yake. 
Msemaji wa polisi ya Dortmund, Nina Vogt, alisema wachunguzi bado hawafahamu chanzo cha milipuko iliyotokea wakati timu ya Borussia Dortmund ilipokuwa ikijiandaa kuondoka hotelini kuelekea uwanjani kuchuana na Monaco. Polisi imesema inalichukulia tukio hilo kuwa shambulizi. Hata hivyo hakuna dalili kuonyesha ni shambulizi la kigaidi.
Explosion am BVB Bus (Reuters/K. Pfaffenbach) Basi la Borussia Dortmund likionekana hapa baada ya mlipuko karibu na hoteli ya timu hiyo kabla mechi
Dortmund iliamua kuiahirisha mechi hiyo ya duru ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kuutangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Twitter ikiongeza kuwa tiketi zote za mashabiki waliotaka kuutazama mtanange huo zinabaki kuwa halali na zitatumika leo.
khamisimussa77@gmail.com

Posted in

Spread the love

NI USIKU WA SCHOLASTTICA

 
 Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyezikusanya Sekunde zikawa dakika, dakika zikawa Saa, saa zikafanya siku zilizounda wiki kisha zikawa mwezi kabla ya mwaka, kalne au jubilee. Nakushukuru  kwa dhati kwa wema na mapenzi yako Mungu uliyeichagua tarehe ya leo kutimiza miaka kadha ya umuri wangu. Aidha nakuomba uwahurumie wazazi wangu, ambao uliwateua kua sababu ya mimi kuja ulimwenguni, kama walivyonihurumia nilipokuwa mtoto. Walipe malipo mema kwa wema wao kwangu na uwajaliye (Amiin). Happy Birthday to Me.

 Mungu ninakuomba kwa huruma yako mzidishie mema baba yangu, Theado Liya aliyetangulia mbelea ya haki na umpumzishe katika nyumba yake ya milele, apumzike kwa amani na mwanga wa milele umpe eebwana. (Amiin)
 Mungu ninakuomba kwa huruma yako mzidishie mema mama yangu mzazi, Agnes Nasoro umuri mrefu katika Dunia umuondolee maradhi (Amiin). (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
khamisimussa77@gmail.com

Posted in

Spread the love

MAHAFALI YA KWANZA YA TAASISI YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI TANZANIA YAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM




Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Elizabeth Titus Munthali, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Honest Amedeus Matem, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Annastacia Mbunda, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Salim Ngailo, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Lauden Cheyo, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Charles Peter Moshi, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Jengo la Kibiashara la Haidary Plaza jijini Dar es Salaam, leo. 

Baadhi ya Wahitimu wakifuatilia Hotuba ya mgeni rasmi.

Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.akizungumza wakati wa maafali hayo.

Meza Kuu.

Rais wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, akisoma hotuba yake wakati wa maafali hayo.

Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.akitoa neno la shukrani katika maafali hayo.

Sehemu ya ndugu na marafiki wa Wahitimu wakiwa katika maafali hayo.

Mtoa mada katika maafali hayo, Gabriel Mwero, akitoa mada.

Baadhi ya Wahitimu waliopokea vyeti katika mahafali hiyo,wakimsikiliza mgeni rasmi.

Mkaguzi Msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi, akitoa mada katika mahafali hiyo.

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, (kulia) akiteta jambo na Rais wa Taasisi hiyo ya Usimamizi wa Vihatarishi, Pius Maneno, wakati wa hafla hiyo ya maafali katika ukumbi wa Hydary Plaza.

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wahitimu wa Taasisi hiyo.
CCM Blog

Posted in

Spread the love