POLISI WAPONGEZA VIWANGO VYA MAFUNZO YA KAMPUNI YA ULINZI DAR ES SALAAM

OCD Jiliyo Simba alikuwa mgeni rasmi katika gwaride la kufuzu mafunzo ya maofisa 75 ambao wamekamilisha mafunzo ya msingi ya ulinzi katika sherehe  zilizofanyika siku ya jumamosi tarehe 29, Julai 2017 katika kituo cha mafunzo cha SGA kilichopo Mbezi Beach. 

Maofisa 75 tu ndio waliofuzu mafunzo kati ya 179 ambao walikuwa wanapatiwa mafunzo, jambo linaloonyesha viwango vya juu vya mafunzo ambapo waliobakia wataendelea na mafunzo. 


Vilevile OCD Simba  alikagua vifaa ya kampuni ikiwemo magari ya dharura, magari ya zima moto na chumba cha mfumo wa kuongoza mawasiliano. Alifurahishwa na uwekezaji uliowekwa na kampuni hiyo na udhibiti ambao uko katika utendaji kazi wao, hasa mfumo wa kufuatilia.

Maneja Rasilimali watu wa  (HRM) Ebenezer Kaale, alieleza kuwa mafunzo hayo yalikuwa yanajumuisha vitengo vingi wakiwemo huduma kwa wateja, zima moto, huduma ya kwanza, misingi ya haki za binadamu miongoni mwa vitengo vingi vya muhimu vya kiulinzi. 

“Tunaamini kwamba tumewapatia mafunzo ya msingi ya ulinzi kuweza kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi”, alisema. 

Kabla ya kuajiri,  mchujo na uchunguzi wa kina wa maombi yote. Alama za vidole huchukuliwa kwaajili ya kukagua taarifa za makosa kwa maofisa wa Wizara ya  Mambo ya Ndani huku uchunguzi wa kidaktari hufanyika kwaajili ya kukagua uwezo na stamina kabla ya kuanza mafunzo. 

Wakati wa sherehe, wanafunzi waliofanya vizuri walizawadiwa na kupongezwa na mgeni rasmi ambapo waliopongezwa ni walinzi wawili ambao waliweza kuzuia wezi wa mali za wateja wao wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao. 
Ni utamadumi wa kampuni hii ya ulinzi kutambua utendaji wa kiwango cha juu, vyeti na fedha taslimu viliyolewa wakati wa gwaride kuwahamasisha wengine.   
Vilevile alikuwepo RCO SSP wa Kinondoni John Malulu, ambaye alikuwa OCD wa Kawe. Mr Malulu aliipongeza kampuni ya ulinzi ya SGA kwa ushirikaiano iliyokuwa ikitoa wakati akiwa kiongozi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kawe, kwa kusema kwamba ushirikiano wao ulifanya kazi ya upolisi kuwa nyepesi.

Alibainisha kwamba SGA ilitoa magari kwaajili ya doria siku za mwisho wa wiki na siku za sikukuu na kusaidia polisi katika kufanya ukarabati baadhi ya magari yake. 
“SGA ilikuwa ya kwanza kuitika wateja wao na majirani zake na hiyo ilisaidia kupunguza kiwango cha uhalifu. Ninatarajia msaada na ushirikiano wenu katika nafasi yangu mpya.” Aliongeza. 

Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya SGA bwana Eric Sambu, amesema kwamba kampuni hii ni kubwa kuliko zote hapa Tanzania, na inatilia mkazo katika mafunzo kuwapa uwezo wafanyakazi wao kuweza kutekeleza majukumu yao, ili kuweza kufikia na kuzidi matarajio ya wateja wao. 
“mafunzo kwetu mi kiungo muhimu katika mafanikio yetu na tunatilia mkazo kila aina ya wafanyakazi nchini.”, aliongeza.
Walihitimisha jana mafunzo mengine kwaajili ya timu ya ukaguzi wa fedha ya ndani kwajili ya ISO 9001: 2015, kuhusu Udhibiti wa Ubora, ambayo kampuni hii ithibitishwa tangu 2001. 
Kampuni ya ulinzi ya SGA inatoa huduma ya ulinzi, kusafirisha fedha, ulinzi kwa njia ya mitambo ya kielektroniki, huduma ya muito kwa alarm, huduma ya kufuatilia vyombo vya moto, usafirishaji wa mizigo pamoja na kazi zingine.
Inaendesha pia shughuli zake nchi nzima na ina wafanyakazi wapatao 5,000 na wateja kutoka katika kila sekta ya uchumi. 
Baadhi ya viongozi wakisikiliza

Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi Joakim Sabana akizungumza kwenye hafla hiyo.

Baadhi ya viongozi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, wakiimba wimbo wa Taifa

Baadhi ya viongozi wakitambulishwa.

Askari wa kampuni hiyo wakijiweka tayari kabla ya ukaguzi wa gwaride.

0 comments:

Post a Comment