ASHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA LEO


 Kanaeli Urio, asheherehekea siku yake ya kuzaliwa leo nyumbani kwake Kigamboni
 

Mungu mzidishie maisha mema kiumbe wako huyu, Kanaeli Urio (kushoto) ni
 Mama mwenye kuijali familia yake na kuwa na hazina ya upendo kwa kila rika
mama mwenye silaha kubwa ya upendo  utakao muweka katika ramani ya ubinadamu na kauli njema,  niwazi Mmiliki wa ujijirahaa blog anaungana nawe katika kusheherehekea siku ya kuzaliwa na kuzidi kutowa  pongezi kwa wako wazazi walokuzaa na kukulea vyema na kufikia hapo ulipo, Dua sala kwa maombi kuzidi kuwaombea popote walipo wazazi wako sambamba na Mr , ukarimu uwe jadi yako kwa kila rika. (Amiin). (PICHA NA KHAMISI MUSSA)

USIKU WA PENDO NA BINAGI ULIVYOFANA

Jana ijumaa March 17,2017 kuamkia leo jumamosi, ilikuwa ni siku muhimu kwa Malikia wa nguvu, Pendo Kisaka, ambapo ndugu, jamaa na marafiki zake walijumuika naye kwenye Sendoff yake kuelekea kwenye ndoa anayotarajiwa kufunga na mwanahabari/ mwanablogu, George Binagi, March 26,2017 Jijini Mwanza.

Shughuli ilifanyika katika ukumbi wa Heinken, Mbagala Kijichi Jijini Dar es salaam. Ni mwendeleo wa kuelekea kwenye ndoa takatifu ya wawili hao iliyotangazwa March 12,2017 kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
BMG
Bibi harusi mtarajiwa akimvisha saa mmewe mtarajiwa
Bibi harusi mtarajiwa (kulia) na best lady wake (kushoto)
Bibi harusi mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake na kusema ahsante kwa malezi yenu bora
Bibi harusi mtarajiwa, Pendo Kisaka (katikati), akimtambulisha mmewe mtarajiwa, George Binagi (kushoto)

JK AZINDUA TAASISI YAKE YA KUSAIDIA JAMII DUNIANI

 Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hotel ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro Dar es Salaam leo. Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Jakaya Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na mambo mengine  itajihusisha na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini, Afrika na Duniani.
 Kikwete akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi yake ya JMKF
 Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania, Charles Stith
 Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo, Mfanyabiashara maarufu Mtanzania aishie Marekani, Genevieve Sangudi
 Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo ya Wadhamini , Dato' Sri Idris Jala, Waziri asiye na Wizara Maalumu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Pamendu) nchini humo.
 Mwenyekiti wa JMKF, Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taasisi hiyo.
 Jakaya akijadiliana jambo na Balozi Charles Stith
 Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo.
 Jakaya Kikwete akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Taasisi hiyo

 Dato' Sri Idris Jala kutoka Malaysia
 Genevieve Sangudi kutoka Marekani
 Mwanasheria Maarufu nchini, Balozi Mwanaidi  Sinare Maajar. Alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza 2006 na Marekani 2013



 Daktari Bingwa wa Upasuasi, Profesa Wiliam Mahalu
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa  Rwekaza Mukandara
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni la SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa
 Balozi wa zamani wa Marekani nchini, Charles Stith

MWANAMITINDO KHADIJA MWANAMBOKA AADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUJUMUIKA NA MARAFIKI

Wakati Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla zikiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jana, Mwanamitindo nguli hapa nchini na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vitu Vya Khadija, Bi Khadija Mwanamboka aliungana na wanawake wengine jijini Dar es salaam katika kuisherehekea siku hiyo muhimu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanamboka alisema kuwa aliamua kuwaalika marafiki zake katika siku hiyo ili kuwataarifu mpango wake mpya alioupata kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Sense International la nchini Uingereza lenye nia ya kuwasaidia watoto wenye ulemamu wa kusikia na kuona kwa pamoja waliopo hapa nchini, ambapo wataanzisha kitu kinaitwa Pendeza Kids Collection kwa kubuni mavazi mbalimbali ambayo yatauzwa katika Duka la Shirika hilo la Sense lililopo nchini Uingereza na zingine zitauwa hapa hapa nchini ili kuwasaidia watoto hao.

Hafla ya kuisherehekea siku hiyo adhimu kwa kina mama, ilifanyika katika Ukumbi wa Kamarambezi, Sea cliff jijini Dar es salaam.
Khadija Mwanamboka (kati) akiwa na Marafiki zake waliofika kumuunga mkono katika mpango wake mpya wa kuwasaidia Watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona alioshirikiana na Kam
Sehemu ya Marafiki wa Khadija Mwanamboka waliohudhulia hafla hiyo.