WASIA NA LAILA WAMEREMETA KATIKA HARUSI YAO ILIYOFANYIKA HOUSTON, TEXAS NCHINI MAREKANI


Alhamis tarehe 29/12 Bw. Wasia Maya kutoka mjini Houston , Texas aliamua kuachana na kambi ya makapera na kufunga ndoa na Bi. Laila Martin.  Harusi hiyo ilifanyika nyumbani kwa Bw. Wasia na kuhudhuriwa na Watanzania wengi waishio katika jiji la Houston na miji ya jirani. Ijumaa ya tarehe 30/12 kulifanyika Nikka Dinner katika ukumbi wa Pakwan uliopo kwenye makutano ya barabara za HW6 na Beechnut . 
Endela kuona picha za Harusi na Nikka Dinner hapa chini
Maharusi wakiwa na sura za furaha 
Bw. Wasia na mkewe Bi. Laila
Bibi Harusi Bi. Laila


Bw. Wasia

Bi. Laila


MAJONZI: MPOKI BUKUBU AZIKWA NYUMBANI KWAO, MSALATO MJINI DODOMA

01
Alice Mama wa Marehemu Mpoki Bukuku akisaidiwa kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye Mpoki Bukuku wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma Marehemu Mpoki alifariki hivi karibuni jijini Dar es salaam kwa kugongwa na gari maeneo ya Mwenge.
1
Watoto wa Marehemu Mpoki Bukuku Junior akiongozana na wadogo zake wakiweka shada la maua katika kaburi la baba yao wakati wa mazishi yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma.
2
Junior akiwa ameshikili msalaba kwa majonzi wakati wa mazishi ya baba yake.
3
Mke wa Marehemu Mpoki Bukuku Bi. Lilian na watoto wake wakiaga mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
4
jeneza lenye Mwili wa marehemu Mpoki Bukuku likiteremshwa  kaburini.
5
Mbunge wa Singida Mashariki Mh Lazaro Nyalandu akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Mpoki Bukuku.
6
Mke wa Marehemu Bi Lilian akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu mumewe.
7
8
Viongozi wa Dini wakiwa katika ibada hiyo ya mazishi.
9
Ndugu na jamaa waombolezaji wakiomboleza kwa uchungu mkubwa.
10
12
Naibu Waziri Anthony Mavunde pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Mh. Razalo Nyalandu wakiombea mwili wa  marehemu Mpoki Bukuku.
13
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
16
Junior akiaga mwili wa baba yake Marehemu Mpoki Bukuku.
17
18
Mama wa Marehemu Mama Alice akiaga mwili wa mtoto wake mpendwa marehemu Mpoki Bukuku.
19
Waombolezaji wakiwa katika mstari wa kuaga mwili wa marehemu.
20
Naibu Waziri Anthony Mavunde pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Mh. Razalo Nyalandu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa  marehemu Mpoki Bukuku.
21
Naibu Waziri Anthony Mavunde akitoa salam za pole kwa wafiwa.
22
Naibu Waziri Anthony Mavunde akisaini kitabu cha maombolezo.
23
Mpiga picha wa magazeti ya Serikali TSN Habari Leo na Dairly News Bw. Mroki Mroki akitoa salamu za pole kwa wafiwa kwa niaba ya chama cha wapigapicha.
24
Bw. John Bukuku akitoa salamu za pole kwa wafiwa kwa niaba ya Wanamitandao
25
Mwenyekiti wa Press Club ya waandishi wa habari mkoani Dodoma Bw. Chidawali akitoa salamu zake kwa niaba ya wanahabari mkoani humo.
26
Mbunge wa Singida mjini Mh. Lazaro Nyalandu akitoa salam za pole kwa wafiwa.
27
Waombolezaji wakiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.

MWIMBAJI MAARUFU WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AFUNGA PINGU ZA MAISHA

Mbali ya kuwa Sikukuu ya Krismasi kwa Wakristo duniani, pia jana Disemba 25,2016 ilikuwa siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine (wawili katikati), baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.

Bibi harusi ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Jijini Mwanza, akifahamika zaidi kwa jina la Agnes Akrama, wote wakimtumikia Mungu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. Picha na Craty Cleophace
Maharusi na wasaidizi wao, wakimsikiliza Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpywa, Dkt.Daniel Moses Kulola, wakati wa ibada yao
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo wakati wa ibada ya ndoa
Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine, wakila kiapo cha ndoa.

"Mungu akasema, Si vyema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Mwanzo 02:18
BMG inawatakia maisha mema, Amen!
Tazama picha zaidi HAPA

NDOA YA GODFREY SINYANGWE NA ESTHER KILUMA WA JIJINI MWANZA YAFANA

Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma wakivishana pete ya ndoa
Upendo wa dhati
Bwana Godfrey Sinyangwe (kushoto) na Bibi Esther Kiluma, wakifurahia ndoa yao
Wanapendana sana
Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma
Ndoa na iheshimiwe na watu wote
Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma wakiwa ufukweni
Ndoa yetu na idumu milele
Baada ya ndoa pamoja na zoezi la kupiga picha katika ufukwe wa ziwa Victoria, shughuli usiku huu inafanyika Ukumbi wa Bugando Club.

SAFARI YA MWISHO YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KATIKA KITUO CHA KIBO KABLA YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU

Baada ya kupuumzika kwa siku mbili katika kituo cha Horombo kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ,safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo ikaanza .
Safari ilivyoendelea hali ya hewa ilibadirika arikadhalika uoto wa misitu mifupi ulianza kutoweka kadri safari ilivyoenedelea.
Safari iliendelea kwa motto wa "Mdogo Mdogo".
Wakati mwingine  kulihitajika maneno ya faraja ili kufanikisha safari hii.
Eneo hili ndilo la mwisho katika Mlima Kilimanjaro kuona maji yakitiririka wakati wa safafri ya kupanda Mlima Kilimnjaro.
Kutokana na kubadirika kwa hali ya hewa ,washiriki wengine walivalia vizuia upepo,wenyewe walivipa jina "Shilawadu".
Baadae uoto wa misitu ukatoweka kabisa ,safari ikawa ni ya kupita katika eneo la jangwa likijulikana kama Saddle.
Safari iliendelea ya kufika kituo cha mwisho cha Kibo Hut.
Wenye kuhitaji Msaada ,walipata msaada.
Mapumziko kwa ajili ya kupata Chakula yalifanyika katika eneo la Saddle.
Safari iliendelea ikiambatana na mvua katika eneo la Jiwe la Okoyo.
Hatimaye Safari ya kutoka kituo cha Horombo ikafikia tamati katika kituo cha Kibo Huts.
Washiriki wakapata picha ya pamoja  kabla ya kupata mapumziko kujiandaa na sfari ya kuelekea Kileleni itakayofanyika majira ya saa 5 usiku. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.