MTANZANIA ALIYEIBUKA MSHINDI WA KWANZA AFRIKA NA WA SITA DUNIANI KATIKA MASHINDANO YA KUSOMA QUR-AN KWA NJIA YA TAJIWEED AWASILISHA TUNZO KWA MZEE MWINYI LEO

 Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakary Bin Zubeir (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), wakati wakimsubiri kumpokea, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kuwasili kwenye Ofisi za Bakwata Kinondoni Jijini Dar es Salaam, leo katika hafla ya kumpongeza Mwanazuoni kutoka Kondoa,Tanzania, Sheikh Rajay Ayub ambaye ameibuka mshindi wa kwanza Afrika na wa sita Duniani katika mashindano ya 37 ya Kimataifa ya usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed, yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Iran. Zifuatazo ni picha kem kem za hafla hiyo.


UHURU FM YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI VYA SH. MILIONI 3 KWA CHUO CHA VETA CHA WENYE ULEMAVU CHA YOMBO, DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akiwa na badhi ya wafanyakazi wa Radio hiyo, wakati yeye na wafanyakazi hao walipowasili kwenye Chuo cha VETA  cha wenye ulemavu kilichopo Yombo Kata ya Kiwalani Temeke Dar es Salaam, kutoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo ni pamoja na Mchele, unga, saruji, sabuni kasha la huduma ya kwanza, mifagio, mafuta ya kula, kofia maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, miwani, viti, mafuta maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, vifaa vya michezo ambavyo ni jezi za mpira wa miguu na netiboli, mipira ya kawaida na mipira ya kengere kwa wenye ulemavu wa macho, Kamba ya kuvuta kwa ajili ya walemavu, vyote vyenye thamani za zaidi ya sh. milioni 3.  zifuatazo ni picha mbalimbali kuhusiana na tukio hilo.