Padri wa Kanisa la Roman Cathoric, Parokia ya Watakatifu Wote Kiloleli Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza, akiongoza ibada ya maombi ya kuuaga mwili wa Marehemu, Mzee Pius Joseph Mkunja, Mzaliwa na Mkazi wa Mpanga Kilombero Mkoani Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika jana kanisani hapo.
Mzee Mkunja alifariki dunia juzi April 25,2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza akikokuwa akipata matibabu. Alizaliwa Mwaka 1926 hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 90. Kifo chake kimetokana na tatizo la vidonda vya tumbo. Alikuwa mfanyabiashara maarufu enzi za uhai wake.
Mwili wake unasafirishwa hii leo April 27,2016 kuelekea nyumbani kwake Mpanga, Kilombero Mkoani Morogoro kwa ajili ya Mazishi.
Tunatoa natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu, akiwemo mtoto wa Marehemu, Bi.Idda Adam.