MANENO MBEGU NA QUEEN SENDIGA WAMEREMETA

 Bwana Harusi Maneno Mbegu akivishwa pete na mwandani wake, Queen Sendiga walipokuwa wanafunga ndoa hivi karibuni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
                     Maneno Mbegu akiapa mbele Ofisa Tawala  Wilaya ya Kinondoni
                                    Queen akila kiapo
                                Mbegu akitia saini
 Queen akitia saini
Wakitoka baada ya kufunga pingu za maisha
Du! hivi kweli tumeoana?
                                                Maharusi wakiwa na sura za bashasha
Huyu ndiye Mbegu
Baba akimpongeza binti yake kwa kuolewa
Mbegu na mkewe Queen akiw na katika picha ya pamoja na wakwe zake.
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao pamoja na marafiki

Quenn anavyomeremeta
Queen akiwa na mamake mzazi katikati na mdogo wake
Queen akiwa na watoto wapambe

ZIARA YA WASSIRA WILAYANI MAGU MKOANI MWANZA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wasira akiwa na Mkuu wa wilaya ya Magu, Jacqueline Liana alipokagua maendeleo ya  katika shule moja akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza tarahe 24. 7. 2013

 Waziri na Mkuu wa wilaya, wakishuhudia mmoja wa wananfunzi wa shule hiyo alipokuwa akiandika ubaoni

 Waziri akizungumza na wanafunzi katika shule hiyo
 Waziri Wasira akiwapongeza wananfunzi wa shule hiyo
 Waziri Wasira akikalia moja ya viti vilivyotengenezwa na mafundi wajasiriamali  wa viti hivyo katika wilaya hiyo ya Magu.
 Kinamama wakicheza ngoma kunogesha ziara hiyo ya waziri Wasira
 Waziri Wasira akizungumza na wananchi katika ukumbi wa shule wilayani Magu. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Magu, Jacqueline.
 Waziri Wasira akiwaslimia kinamama
 Waziri Wasira akikagua moja ya miradi ya ujenzi katika wilaya hiyo
 Waziri Wasira akishauliana jambo na viongozi wa wilaya hiyo
 Kikundi cha ngoma cha vijana wa wilaya ya Magu wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngom,a wakati wa ziara hiyo.
Kijana akipambana na nyoka aina ya Chatu aliyekuwa akicheza naye ngoma wakati wa ziara hiyo. PICHA KWA HISANI YA MKUU WA WILAYA YA MAGU, JACQUELIN LIANA

BENKI YA DUNIA YAIPA CHANGAMOTO AFRIKA KUBORESHA MATUMIZI YA ARDHI KUONDOA UMASIKINI

WASHINGTON, DC, Julai 22, 2013 – Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.


Ripoti ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013  imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni  202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta mafanikio kwa jumla.
Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki  wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika,
Ripoti  hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia  47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola za Marekani $1.25 kwa siku..

“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,”  anasema  Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
“Kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.”

Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..

Mpango wa kuleta mabadiliko

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake  katika kipindi cha muongo ujao kwa::· Kuwa na mabadiliko  na uwekezaji kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi. · Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika.  .· Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa  usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao  kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini. · Serikali za Afrika kuwa na dhamira  ya kisiasa  kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .

Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5  katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji